Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka viongozi wa Cyprus kufanya kazi zaidi ili kufanikisha mkutano wa kimataifa juu ya hatma ya taifa hilo

Ban awataka viongozi wa Cyprus kufanya kazi zaidi ili kufanikisha mkutano wa kimataifa juu ya hatma ya taifa hilo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa hakuna maendeleo yoyote yaliyopigwa kuhusiana na ufufuaji wa mazungumzo ya kusaka suluhu ya kudumu baina ya maeneo ya Ugiriki na Uturuki ambayo yaliyopo kwenye mzozo juu ya uhalali wa sehemu moja kuwa na miliki ya ardhi.

 Ban amewaambia viongozi wa makundi ya jamii ya Cyprus walioko Ugiriki na wale wanaishi nchini Uturuki kuwa hakuna maendeleo ya kutosha yaliyopigwa ambayo yatawezesha kufanyika kwa kongamano la kimataifa kwa ajili ya kuyagawanya mataifa hayo yaliyoko kwenye kisiwa cha Mediterranean.

Amejadiliana kwa kina na viongozi hao na amewaarifu kuhusu kutofikiwa kwa muafaka juu ya masuala nyeti ambayo yanapaswa kwanza kutatuliwa kabla ya kufanyika kwa mkutano huo.

Amewahimiza viongozi wote kuchukua hatua madhubiti na hatimaye kukubali kuchukua maamuzi magumu kwa mustakabali wa taifa hilo la Cyprus.