Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yakaribisha uamuzi wa mahakama kuu nchini Kenya

UNAIDS yakaribisha uamuzi wa mahakama kuu nchini Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS limeipongeza mahakama kuu nchini Kenya kutokana na uamuzi wake wa kuhakikisha kuwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi wamepata madawa yaliyo nafuu.

Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe ameutaja uamuzi huo kuwa wenye umuhimu kwa kuwa idadi kubwa ya watu nchini Kenya wanayategemea madawa hayo. Kwenye mataifa yenye kipato cha chini zaidi ya asilimia 80 ya madawa ya Ukupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi yanayotumiwa na watu milioni 6.6 yanatoka kwa watengezaji wa madawa ya kijeneriki ambapo watu milioni nane walikuwa wakipata matibabu hadi mwaka 2010.