UNRWA na OCHA walaani kutawanywa kwa nguvu wakimbizi wa Kipalestina

23 Aprili 2012

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA wamesema wiki hii wakimbizi wa Kipalestina 67 nusu yao wakiwa ni watoto wametawanywa kwa nguvu kutokana na kuhamishwa au nyumba zao kubomolewa kwenye Ukingo wa Magharibi.

Mashirika hayo mawili yanasema katika tukio moja uongozi wa Israel ulibomoa nyumba za familia saba za wakimbizi kwenye jamii ya Wapalestina ya Al Khalayeleh ikiwalazimisha kutawanyika kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi sita. Na siku iliyofwata uongozi wa Israel ukabomoa na kuchukua mahema yaliyotolewa na mashirika ya misaada ya kibinadamu. OCHA na UNRWA wamelaani vikali hatua hiyo. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud