Suala la Darfur bado ni la kutia hofu jumuiya ya kimataifa

23 Aprili 2012

Suala la Darfur bado ni la kutia hofu jumuiya ya kimataifa amesema balozi wa Ufaransa nchini Sudan Patrick Nicoloso wakati ambapo ujumbe wa mabalozi kutoka nchi wanachama wa Baraza la Usalama Sudan walipozuru El-Fasher mji mkuu wa Darfur Kaskazini mwishoni mwa wiki.

Mabalozi hao walikuwa Darfur kwa ajili ya mkutano na kupata taarifa kuhusu hali ya jimbo hilo na pia kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Darfur.

Balozi Nicoloso amesema kila nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa anaunga mkono muafaka wa amani ya Darfur uliotiwa saini Doha Qatar.

(SAUTI YA PATRICK NICLOSO)

Wakati wa ziara yao wajumbe hao walipewa taarifa na maafisa wa serikali, uongozi wa jimbo la Darfur na pia uongozi wa juu wa mpango wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter