Dunia inahitaji huduma za afya na hususan vijana:Ban

23 Aprili 2012

Vijana wana matumaini makubwa ya baadaye lakini hawawezi kuishi kwa matumaini tu, wanahitaji chakula, ajira na huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon Jumatatu katika ufunguzi wa tume ya idadi ya watu na maendeleo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Ban amesema vijana wanahitaji hasa huduma za afya ya uzazi kwa ukweli hauwezi kupuuzwa. Ameongeza kuwa vijana wengi duniani wanashiriki ngono na kwa sababu hiyo wanaweza kukabiliwa na hatari ya afya zao ikiwemo ukatili wa vitendo vya ngono. Hivyo ameongeza wanahitaji taarifa na uwezo wa kujilinda wenyewe.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Vijana wana matumaini makubwa ya baadaye lakini hawawezi kuishi kwa matumaini tuu, wanahitaji chakula, ajira na huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumatatu katika ufunguzi wa tume ya idadi ya watu na maendeleo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Ban amesema vijana wanahitaji hasa huduma za afya ya uzazi kwa ukweli hauwezi kupuuzwa.

Ameongeza kuwa vijana wengi duniani wanashiriki ngono na kwa sababu hiyo wanaweza kukabiliwa na hatari ya afya zao ikiwemo ukatili wa vitendo vya ngono. Hivyo ameongeza wanahitaji taarifa na uwezo wa kujilinda wenyewe.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud