Gharama za uingizaji chakula na mafuta katika nchi masikini zinapanda:UNCTAD

23 Aprili 2012

Kuendelea kupanda kwa gharama za mali asili na bidhaa za kilimo zinaongeza adha ya muda mrefu na kuumiza nchi masikini hasa kupitia kuongezeka kwa bei ya mafuta na chakula badala ya kuzisaidia kutokana na kukusanya mapato ya bidhaa zao wanazosafirisha nje.

Hii ni matokeo ya ripoti ya mwaka 2012 ya bidhaa na maendeleo ambayo ni mpya na iliyochapishwa Jumatatu na tume ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo ya kilimo UNCTAD kwenye kongamano la kimataifa la 13 linaloendelea mjini Doha Qatar.

Ripoti hiyo inasema kuumba kwa soko la bidhaa na ongezeko la gharama za ardhi ya kilimo, mafuta hata mazao ya chakula vimechangia mabadiliko makubwa ya bei za bidhaa ambazo nyingi zinaendelea kupanda. Moja ya nchi masikini zinazohudhuria kongamano hilo ni Uganda inayowakilishwa na waziri wa biashara na ushirikiano David Wandendeya Wakikona. Anazungumzia changamoto zinazowakabili na nini UNCTAD inaweza kufanya kusaidia.

(SAUTI YA WAZIRI DAVID WANDENDEYA)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter