Baraza la Usalama larejea kulaani vikali mapinduzi ya kijeshi Guinea Bissau

21 Aprili 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Guinea Bissau kurejea katika taala wa katiba kufuatia mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita. Baraza pia limetaka kuachiliwa mara moja kwa Rais wa mpito, waziri mkuu na maafisa wengine waliowekwa mahabusu. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice ni rais wa baraza kwa mwezi huu wa Aprili.

(SAUTI YA SUSAN RICE)

Baraza la Usalama linakaribisha uamuzi wa baraza la amani na salama la Muungano wa Afrika kuisitisha mara moj uanachama wa Muungano wa Afrika Guinea Bissau hadi pale masuala ya katika na utulivu utakaporejeshwa.

Baraza linasisitiza haja ya kuhakikisa usalama wawale wanaoshikiliwa na kwamba wale wanaohusikana vitendo vya ghasia lazima wawajibishwe.”

Baraza la usalama na Katibu Mkuu wa Umoja wa matauifa wamelaani vikali mapinduzi nchini humo ambayo yalifanyika wakati duru ya pili ya uchaguzi wa Rais ilipangwa kufanyika Aprili 22.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter