UNCTAD inaweza kuweka msingi muafaka wa maendeleo baada ya matatizo:Migiro

21 Aprili 2012

 

UNCTAD inaweza kuweka msingi muafaka wa maendeleo baada ya matatizo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu kwenye ufunguzi wa mkutano wa 13 wa Umoja wa Mtaifa wa biashara na maendeleo ulioanza leo mjini Doha Qatar.

Katika ujumbe huo uliowasilishwa kwa niaba yake na naibu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro unasema kongongamano hilo umefanyika wakati muafaka kujadili mikakati muhimu ya kukabiliana na hali ya sasa ya utandawazi.

Bi Migiro ameongeza kwamba matatizo makubwa ya kiuchumi yaliyoikumba dunia hivi sasa tangu miaka ya 1930 yanamliza miaka kadhaa ya ukuaji wa uchumi na yanadhihirisha wazi hatari iliyopo katika masoko ya fedha duniani.

(SAUTI YA ASHA MIGIRO)

Wakati mdororo ulianzia katika nchi nyingi zilizoendelea kiuchumi atharin zake zimeikumba dunia nzima na zinaendelea kuathri matarajio ya maendeleo ya nchi nyingi masikini.Tangu wakati huo ufufuaji uchumi umekuwa ukilegalega na kuendelea kuyumba katika nchi nyingi”

Bi Migiro ameongeza kuwa kongamano la 13 la UNCTAD lazima liangalie sababu za matatizo na kubaini hatua za kuzuia yasitokee tena.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud