Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laanzisha mpango wa usimamizi UNSMIS Syria

Baraza la Usalama laanzisha mpango wa usimamizi UNSMIS Syria

Kikao cha Baraza la Usalama kilichofanyika Jumamosi Aprili 21 kimeamua kuanzisha mpango wa usimamizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria UNSMIS. Mpango huo mwanzo utakuwa ni wa siku 90 utaongozwa na kamanda wa jeshi wa uangalizi na mwanzo utakuwa na jumla ya wanajeshi waangalizi wasio na silaha 300 na baadhi ya raia ili kusaidia kutimiza malengo ya mpango huo.

Baraza pia limeamua kwamba mpango huo utakaopelekwa na tathimini ya Katibu Mkuu hasa kutokana na maendeleo yatakayokuwa yanajitokeza nchini humo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usitishasji mapigano. Pia Baraza limesema UNSMIS itakuwa na wajibu wa kuangalia tuu usitishaji wa mifumo yote ya machafuko kutoka pande zote, kuangalia na kusaidia utekelezaji wa mapendekezo sita ya Kofi Annan.

Baraza limemtaka Katibu Mkuu na serikali ya Syria bila kuchelewa kuhutimisha mpango huo kwa kuzingatia azimio la Baraza Kuu namba 58/82. Na limeitaka serikali ya Syria kuhakikisha na kusaidia mpango wa UNSMIS kutekeleza wajibu wake ipasavyo.