Kongamano la kimataifa la uwekezaji linatafuta njia za kujumuisha uwekezaji wa kimataifa katika maendeleo endelevu

20 Aprili 2012

Uwekezaji wa kimataifa kutoka kwa makampuni mbalimbali na ufadhili wa mataifa tajiri una umuhimu mkubwa wa kutoa mtaji unaohitajika kuzisaidia nchi zinazoendelea kukua. Limesema kongamano la tatu la umoja wa Mataifa la maendeleo ya uchumi na biashara UNCTAD lililoanza April 20 na kumalizika April 23 mjini Doha Qatar.

Kongamano hilo lakimataifa la uwekezaji mwaka 2012 litajadili sera na mikakati inayohitajika katika Nyanja hiyo. Pia linajadili jinsi gani mchanganyiko wa mikakati ya sera za ummna na miradi binafsi inaweza kuchagiza uwekezaji zaidi na wa moja kwa moja katika miradi ambayo italeta maendeleo endelevu katika nchi masikini.

Wakati mdororo wa uchumi hivi karibuni umezifanya nchi nyingi kusitisha au kupunguza msaada wa kimataifa kwa nchi masikini makampuni mengi ya kimataifa yamekuwa na akiba ya kutosha mfano mwaka jana pekee yamewekeza takriban dola trilioni 1.6 katika kupanua wigo wa biashara zao nje. James Zhan ni mkurugenzi wa kitengo cha uwekezaji na biashara cha UNCTAD.

(SAUTI YA JAMES ZHAN)

Kama unavyojua fedha na mali huru zina samani ya zaidi ya dola trilioni 5, lakini zimeweka tuu dola bilioni 100 katika uwekezaji wa muda mrefu ambao ni uwekezaji wa moja kwa moja wan je na mwingi wa uwekezaji huo ni katika nchi zinazoendelea. Baada ya kusema hayo tunajua nchi chache tajiri kama Qatar, Kuwait, Singapore na Uchina wamewekeza katika nchi masikini na watapanua wigo wa uwekezaji wao katika nchi hizo.

Kongamano hilo limewaleta pamoja zaidi ya washiriki 600 kutoka nchi zaidi ya 100, miongoni mwao ni wakuu wa nchi 10,mawaziri zaidi ya 40, wenyeviti na mameneja wa makampuni zaidi ya 100 kutoka kote duniani.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud