UNHCR yaonya juu ya kukosekana ufadhili kuwasaidia wakimbizi wa Syria

20 Aprili 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limeonya juu ya mwendo wa kusuasua juu ya ufadhili wa mafungu ya fedha kwa ajili ya kugharimia shughuli za wakimbizi wa Syria walioko katika nchi za Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq.

Wakati huu kunashuhudiwa makusanyo kidogo ya fedha yakifika wastani wa asilimia 25, na hivyo kuweka katika hali ya shaka shaka shughuli za kuwakirimia wakimbizi hao wanahitaji huduma za dharura.

Kati ya mashirika 34 yaliyotoa mwito kupigwa jeki kupatiwa msaada wa fedha kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao, ni mashirika 8 tu ndiyo yaliyopata ufadhili huo.

UNHCR inasema kuwa nchi zinazohifadhi wakimbizi hao pamoja na mashirika mengine yanayofanya kazi za kuwahudumia zimeanza kuonyesha ishara ya kukata tama.

Licha ya mkwamo huo wa ukosefu wa ufadhili, Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wahisani wake, inaendelea kusambaza miradi mbalimbali kwa wakimbizi hao na jamii zinazowahifadhi kama anavyoelezea afisa wa UNHCR Melisa Fleming .

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter