Mtaalamu huru wa UM kwenda Marekani kufanya tathmini

20 Aprili 2012

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa James Anaya anatazamia kuitembelea Marekani kuanzia April 23 hadi May 4 mwaka huu, katika ziara ya kutathmini hali jumla ya watu wazawa.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwa mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa kulitembelea taifa hilo ambaye pia anatazamia kutoa ripoti yake kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Akijadilia ziara yake hiyo,mtaalamu huyo amesema kuwa atatupia macho ustawi wa watu wanaotambulika kama jamii ya wahindi na wamarekani asilia. Ama atasafiri hadi kule wanakoishi jamii ya watu wa Hawaii na Alaska.

Lakini pia atatembelea maeneo kadhaa ikiwemo Washington DC, Arizona, Kusini mwa Dakota na Oklahoma atakofanya majadiliano na viongozi wa majimbo hayo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud