UNICEF yaipiga jeki Yemen kufanikisha kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa Surua

20 Aprili 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeanza kuipiga jeki serikali ya Yemen ili kufanikisha kampeni ya nchi nzima ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa surua ulioripotiwa kuzuka nchini humo mwaka uliopita.

Katika mpango huo, IOM inashirikiana na wizara ya afya na idadi ya watu na tayari wataalamu kadhaa wameshapatiwa mafunzo ya awali ya jinsi ya kutekeleza kampeni hiyo ambayo inakusudia kufanywa katika maeneo ambayo yamevurugwa kutokana na machafuko ya kisiasa.

Wilaya zilizoko kaskazini mwa nchi hiyo zimekosa utengamao kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kushadidi wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi yanayotaka kulitwaa eneo hilo.

Kampeni ya utoaji chanjo inakusudia kuwafikia jumla ya watoto 126,000 walio chini ya umri wa miaka 10 katika kipindi cha mwezi May.

(SAUTI YA MERIXIE MERCADO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud