Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani kutumika kwa hakama za kijeshi kuhumu kesi za kiraia

UM walaani kutumika kwa hakama za kijeshi kuhumu kesi za kiraia

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu inasema kuwa kuna hali ya kutia wasiwasi juu ya ustawi wa raia nchini Palestina katika ukingo wa Gaza kufuatia kushamiri kwa matukio ya kutolewa kwa hukumu ya vifo huku wengine wakinyongwa.

Kunaripoti pia hukumu nyingi za kifo sasa zinahamishiwa katika mahakama za kijeshi dhidi ya zile za kiraia.

Tangu kuanza kwa mwaka huu mamalaka nchini humo zimetoa hukumu za kifo zisizo pungua sita , na moja kati ya hiyo ilitolewa wakati mhusika wake hakuwepo mahakamani.

Watu watatu walinyongwa hadi kufa April 7 mwaka huu na mwingine kati ya hao waliohukumiwa anaweza kunyongwa muda wowote.

Kamishna hiyo ya Umoja wa Mataifa inapinga matumizi ya vyombo vya kijeshi kuendesha kesi za kirai.

Kuna ripoti kwambam, watuhumiwa wengi katika eneo la Gaza hawapewi fursa ya kuwasiliana na wanasheria wao na mara zote mahakama hizo za kijeshi zinaegemea ushahidi wa upande mmoja.