Hali bado ni tete nchini Syria licha ya kuwepo kwa mpango wa usitishwaji mapigano

20 Aprili 2012

Kukiwa kumepita kipindi cha wiki moja tangu kupitishwa kwa mpango wa usimamishaji mapigano nchini Syria, hali jumla bado ni tete katika eneo hilo na ripoti zinaonyesha kujitokeza kwa matukio ya mashambulizi.

Kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Kofi Annan bado kunashuhudiwa mashambulizi ya hapa na pale ambayo yamesabisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine wakijeruhiwa.

Bwana Annan amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa utashi wa kisiasa unaoonyeshw ana serikali ya Syria ambayo inatoa ushirikiano mkubwa kwa ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa, lakini utengamao wa kweli bado haujapatikana.

Umoja wa Mataifa umetuma ujumbe wa waangalizi 7 wasio askari Mjini Damascus kwa ajili ya kusimamia utekelezaji mpango wa usimamishaji mapigano. Baraza la Usalama linatazamia kukutana hii leo kwa ajili ya kujadilia hatua za kupeleka kikosi kamili nchini humo kitachokuwa na waangalizi wasiopungua 300. Ahmad Fawzi ni msemaji wa ujumbe huo.

(SAUTI YA AHMED FAWZ)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud