Baraza la Usalama lina jukumu muhimu la kukabiliana na tishio la nyuklia:Ban

20 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea jukumu muhimu linalofanywa na Baraza la Usalama katika kukabiliana na tishio la uzalishaji wa nyuklia wakati wajumbe 15 wa baraza hilo walipokutana kutathimini juhudi za karibuni za kimataifa katika upande wa upokonyaji silaha na usalama.

Katika taarifa yake kwa baraza Ban amesema jumuiya ya kimataifa inalitazama baraza la usalama kuendelea na uongozi wa kutoa msukumo wa kisiasa unaohitajika ili kufikia amani na usalama wa dunia kuwa huru bila silaha za nyuklia.

Kikao hicho cha Baraza la Usalama kimefanyika kwa juhudi za Marekani ambaye ndio rais wa baraza kwa mwezi huu na kikao cha kufuatilia kikao kilichoongozwa na Rais Barack Obama mwei September 2009 kuhusu upokonyaji silaha, kutozalisha silaha za nyuklia na usalama.

Kikao hicho kimesema kinatambua haja ya kila nchi kuchukua hatua kuzuia bidhaa za nyuklia au msaada wa kiufundi ambao unawafikia magaidi wanaotaka kutumia nyuklia. Ujumbe wa Marekani kwenye kikao hicho umesema juhudi nyingi zimefanyika tangu mwaka 2009 ili kupunguza hatari ya kimatifa ya silah za nyuklia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter