Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji kutoka Ethiopia wakabiliwa na changamoto za afya Yemen:IOM

Wahamiaji kutoka Ethiopia wakabiliwa na changamoto za afya Yemen:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatiwa hofu na hali ya maelfu ya wahamiaji kutoka Ethiopia waliokwama nchini Yemen kwenye jimbo la Haradh kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Saudia, kufuatia kuzuka  kwa homa ya kidingapopo iliyoanza mwezi uliopita.

Homa ya kidingapopo ni homa itokanayo na virusi vinavyosababishwa na mbu na dalili zake ni kuwa na joto kali, kuumwa kichwa, kuumwa viungo, muwasho wa ngozi na kutokwa na damu na isipotibiwa mapema inaweza kusababisha vifo hasa kwa watoto.

Kwa mujibu wa IOM ingawa hakuna vifo hadi sasa homa hiyo inasababisha matatizo makubwa ya kiafya kwa wahami hao 12,000 waliokwama amba wanajumuisha pia wahamiaji 3000 wa Kiethiopia waliojiandikishwa kwa IOM kurejea nyumbani.

Visa 17 vimesharipotiwa kwenye kliniki ya IOM ya Haradh mwezi huu na wagonjwa watano ni wafanyakazi wa IOM kituo hicho kinatoa msaada wa dharura, kinasaidia kuwasafirisha wagonjwa kwenda hospitali zingine na kutoa ushauri nasaha kila siku kwa wahamiaji kati ya 70 hadi 100.