Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabalozi wema wazindua changamoto na nafasi ya kushinda magari yenye ufanisi

Mabalozi wema wazindua changamoto na nafasi ya kushinda magari yenye ufanisi

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linasema siku ya kimataifa ya mazingira mwaka huu ina malengo makubwa kuliko wakati mwingine wowote. Mabalozi wema wa shirika hilo wamezindua changamoto ambayo inatoa fursa ya watu kujishindia magari yanayotumia mafuta ya ufanisi.

Changamoto ni kwamba watu kote duniani watapewa changamoto ya kuahidi na kutekeleza shughuli za kimazingira kwa ajili ya siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 5 na kusaidia kuvunja rekodi ya kuwa na shughuli nyingi mbalimbali za siku ya mazingira katika historia ya miongo mine.

Katika siku hiyo ya mazingira kampuni ya magari ya Kia Motors itatoa zawadi ya magari matano kwa miradi bora zaidi ambayo itakuwa katika makundi matano ambayo ni moja watu: mradi utakaojumuisha idadi kubwa kabisa ya watu, pili ni kauli mbiu: mradi utakao unga mkono zaidi kauli ya siku hiyo ambayo ni Uchumi unaojali mzingira je unakujumuisha? Tatu mradi utaokuwa na ubunifu zaidi, nne mradi utakaojumuisha kiasi kikubwa cha mawasiliano ya mtandao na mwisho mradi ambao utaleta mabadiliko. Ili kuweza kushiriki miradi yote lazima iwe imeandikishwa kwenye mtandao ifikapo Juni 30 mwaka huu na washindi watatangazwa Julai 30 mwaka huu.