Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya mabomu Iraq yaliyotokea Alhamisi

UM walaani mashambulizi ya mabomu Iraq yaliyotokea Alhamisi

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amelaani vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotokea Alhamisi nchini Iraq ambayo yamekatili maisha ya watu zaidi ya 30 na kujeruhi wengine wengi. Bwana Kobler ameelezea hofu yake kutokana na kuendelea kwa ghasia nchini Iraq na kulengwa kwa maafisa wa majeshi ya usalama, wafanyakazi wa majeshi hayo na mashambulizi ya makundi fulani ya raia.

Amesema uhalifu huo dhidi ya raia wa Iraq lazima ukomeshwe ili kuweza kuwa na amani na mustakhbali ambayo watu wa taifa hilo wanastahili.

Amerejea kutoa wito kwa Wairaq wote kushirikiana kumaliza uasi huo na kukumbatia matumaini ya kuwa na demokrasia na taifa imara. Ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kujeruhiwa.