Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM alaani hatua ya kuwaondosha familia za kipalestina

Afisa wa UM alaani hatua ya kuwaondosha familia za kipalestina

Afisa wa Umoja wa Mataifa ameshutumu vikali hatua ya kuwatimua kwenye maskani zao familia za Kipalestina huko kaskazini mwa Jerusalem. Maxwell Gaylard ametaka usitishwaji mara moja kwa hujuma hiyo kwa vile inakwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Kuondolewa kwa familia hizo kunafuatia hukumu iliyotolewa na mahakama moja, baada ya jamii ya wa Israel kwenda mahakamani. Jamii hiyo ya wa Israel inampango wa kujenga kuanzisha ujenzi wa nyumba kadhaa katika eneo hilo ambalo lipo karibu na eneo linalojulikana Beit Hanina.