Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya mambo Syria ni “ suala nyeti”

Hali ya mambo Syria ni “ suala nyeti”

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema kuwa macho na masikio ya wengi yanapelekwa nchini Syria ambako wengi wanatizama hali hiyo kama “lengo linalotembea”. Barazal hilo la usalama linatazamiwa kupokea mchanganua wa hali ya mambo kutoka kwa mjumbe wake aliyetumwa huko kutathmini hali ya mambo.

Ujumbe wa watu sita tayari uko nchini Syria kufuatilia mpango wa usimamishaji mapigano ulioanza kutekelezwa April 12.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Rais wa baraza hilo la usalama Suzan Rice amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa ya barua kutoka kwa Katibu Mkuu inatazamiwa kuwasili katika kipindi cha muda mfupi baadaye.