Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU inasaidia maendeleo ya Broadband katika nchi za Marekani Kusini

ITU inasaidia maendeleo ya Broadband katika nchi za Marekani Kusini

Kongamano la kikanda la shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya habari na teknolojia ya mawasiliano ITU linafanyika wiki hii mjini Mexico City kujadili maendeleo ya karibuni kwa upande wa broadband likiwashirikisha wakurugenzi wakuu na maafisa wengine wa bodi wa ngazi za juu wakiwakilisha makampuni mbalimbali ya teknolojia ya mawasiliano duniani.

Kongamano hilo maalumu kwa ajili ya nchi za Marekani Kusini limewaleta pamoja pia wadau muhimu kushughulikia tofauti za kidijitali wakiwemo mawaziri wa serikali na maafisa wa ngazi ya juu kutoka nchi za Marekani Kusini wakiangalia kwa kina maendeleo ya miundombinu ya broadband, sera na mikakati kwa aliji ya nchi hizo. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)