Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM atilia shaka hali ya wananchi wa Yemen

Afisa wa UM atilia shaka hali ya wananchi wa Yemen

Katika mkesha wa ziara yake ya siku mbili nchini Yemen, afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake namna hali ya usalama inavyozidi kuzorota nchini humo na kuyumbushina hali ustawi wa kijamii.

Bi Catherine Bragg ametaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kusaidia ustawi wa nchi hiyo ambayo inaandamwa na matukio yanayovuruga usalama jumla.

Amesema mamia kwa maeflu ya watu wanaendelea kuishi maisha ya taabu na dhiki kubwa huku huduma za utoaji wa misaada ya usamaria mwema zikizorota.

Kuna idadi kubwa ya watu wanaokosa huduma muhimu ikiwemo huduma za kiafya, kukosekana kwa maji safi na salama hatua ambayo inazidi kuvuruga ustawi wa taifa hilo.

Ametaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na wananchi wa nchi hiyo ambayo amesema kuwa kwa sasa wanapitia katika kipindi kigumu.