Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za dharua zinahitajika kushughulikia hali kwenye eneo la Sahel:Ban

Hatua za dharua zinahitajika kushughulikia hali kwenye eneo la Sahel:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka jamii ya kimataifa kufanya hima na kutafuta suluhu la hali ilivyo kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika ambapo watu milioni 15 wameathiriwa na ukame pamoja na mizozo. Akihutubia bunge la Luxembourg Ban ameitaka dunia kuchukua hatua akisema kuwa eneo hilo kwa sasa linakabiliwa na uhaba wa chakula, kupanda kwa bei ya mafuta na ukame.

Takwimu zinaonyesha kuwa takriban watu 15 wameathiriwa baada ya watoto 200,000 kufa kutokana na utapiamlo mwaka uliopita huku maisha ya wengine milioni moja yakiwa hatarini hivi sasa. Kulingana na shirika la kuratibu masusla ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA ni kwamba hali inayolikumba eneo la Sahel inazidi kuwa mbaya kila kukicha.