Mkutano kuhusu hali ya kibinadamu kuandaliwa Geneva

18 Aprili 2012

Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva imetangaza kuwa mkutano kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria unatarajiwa kuandaliwa siku ya Ijumaa. Wakurugenzi kutoka kwa idara zinazohusika na masuala ya kibinadamu kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo mjini Geneva.

Msemaji wa Umoja wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva Corinne Momal-Vanian anasema kuwa mkutano huo umepangwa na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA, Muungano wa kislamu na tume ya kibinadamu ya Ulaya. Kwa sasa kundi la waangalizi sita kutoka Umoja wa Mataifa wako nchini Syria kushuhudiwa kusitishwa kwa ghasia baada ya siku ya mwisho tarehe 12 mwezi huu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter