Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaonya juu ya ongezeko la maradhi yatokanayo na vyakula Ulaya na Asia

FAO yaonya juu ya ongezeko la maradhi yatokanayo na vyakula Ulaya na Asia

Unene wa kupindukia na maradhi ya moyo yanaweza kuwa changamoto kubwa ya kiafya kwa bara za Ulaya na Asia ya Kati katika miongo miwili ijayo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO.

FAO imeonya kwamba wakati watu wanakula saana nyama na bidhaa za maziwa kiwango cha magonjwa yanayotokana na vyakula kitaweza kuongezeka katika baadhi ya maeneo ya Ulaya na Asia ya Kati. Matokeo haya yamo kwenye ripoti itakayowasilishwa na FAO kwenye mkutano utakaofanyika nchini Azerbaijan baadaye wiki hii.

FAO inasema ongezeko la hatari ya magonjwa kama unene wa kupindukia na ugonjwa wa moyo yataongeza shinikizo katika mifumo ya afya hususani katika nchi masikini za Asia ya Kati. Ripoti imebaini kwamba ingawa njaa bado ni hali inayotia hofu katika eneo kubwa la Ulaya na Asia ya Kati itakuwa ni tatizo ndogo ifikapo 2030. Inakadiriwa kwamba idadi ya watui watakaokabiliwa na njaa inashuka kutoka asilimia 9 hadi asilimia 2 na kufikia asilimia moja mwaka 2050.