Pillay amezitaka nchi kuingiza masuala ya haki za binadamu katika mjadala wa Rio+20

18 Aprili 2012

Wakati majadiliano ya matokeo ya mkutano wa Rio+20 yakiingia katika awamu muhimu, Kamishina Mkuu wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameyataka mataifa yote wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinajumuishwa katika majadiliano na matokeo yoyote ya mkutano huo.

Miaka 20 baada ya kupitishwa azimio la Rio, mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu unatarajiwa kufanyika Juni mwaka huu. Kwa masikitiko Bi Pillay amesema barua iliyotumwa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mswaada wa matokeo ya mkutano wa Rio+20 umeshindwa kutoa uzito kwa masuala ya haki za binadamu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud