Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na Wizara ya Afya Syria kuendesha kliniki za dharua

WHO na Wizara ya Afya Syria kuendesha kliniki za dharua

Shirika la aAfya duniani WHO kwa ushirikiano na wizara ya afya na jumuiya ya mpango wa uzazi ya Syria wanaanzisha kliniki za dharura za kwenye magari katika maeneo ambayo vituo vya afya havifanyi kazi tena kutokana na machafuko yanayoendelea.

WHO na washirika wengine wa afya wamekutana na chama cha msalaba mwekundu cha Syria SARC ili kubaini miradi ya afya ambayo inahitajkika haraka.

Mfuko wa msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF metoa dola milioni moja kwa shirika la WHO ili kuendelea na kazi zake nchini Syria.