Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa umezindua mpango mpya wa kutathmini hatari mijini

Umoja wa Mataifa umezindua mpango mpya wa kutathmini hatari mijini

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari ya majanga UNISDR Jumatano imezindua mpango mpya kusaidia miji kote duniani kukabili hatari kufuatia mwaka mbaya zaidi ulioghubikwa na hasara za kiuchumi zilizosababishwa na majanga.

UNISDR pia imetangaza kwamba miji zaidi ya 1000 sasa imejiunga na kampeni ya kuifanya miji kuwa imara.

Mkurugenzi wa kampeni hiyo Helena Molin Valdes amesema majiji na miji iko msitari wa mbele katika upunguzaji wa hatari ya majanga na ndiyo inayobeba hasara zitokanazo na majanga hayo. Amesema mwaka jana pekee hasara ilikuwa dola bilioni 380. Ameongeza kuwa mpango huo umezinduliwa ili kubaini mipango na mapungufu ya uwekezaji katika upunguzaji wa hatari ya majanga na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)