Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri yadhamiria kuwachanja watoto milioni 12.5 katika kampeni ya Polio

Misri yadhamiria kuwachanja watoto milioni 12.5 katika kampeni ya Polio

Misri itazindua kampeni ya siku nne ya chanjo ya Polio April 21 ikiwalenga watoto milioni 12.5 walio chini ya umri wa miaka mitano wamesema maafisa wa serikali ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Amr Qandeel naibu waziri wa afya anayehusika na dawa za kinga, chanjo ni muhimu sana kutokana na sera za serikali za kuwachanja watoto dhidi ya magonjwa hatari kama Polio. Waziri Qandeel amesema wametoa wito kwa wazazi wote kujitokeza katika vituo vya afya ili kuruhusu watoto wao kupata matone ya chanjo.

Misri ilitangazwa kuwa huru bila ugonjwa wa polio mwaka 2006 baada ya kuorodhesha kisa cha mwisho mwaka 2004. Kampeni hii itaigharimu serikali dola milioni 5 na kuhusisha wahudumu wa afya 800,000.