Waangalizi wa UM waanza kazi yao nchini Syria

17 Aprili 2012

Kundi la kwanza la waangalizi wa Umoja wa Mataifa liko nchini Syria kuanza kazi yake. Waangalizi hao wasiojihami watawasilisha matokeo yao kwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kaiarabu Kofi Annan.

Msemaji wa kundi hilo Kieran Dwyer anasema kuwa waangalizi hao wamekuwa wakikutana na utawala wa Syria na pia upinzani kuhakikisha kuwa kila upande umeelewa wajibu wake. Dwyer ameongeza kuwa ifikapo mwishoni mwa juma waangalizi 30 wataingia nchini Syria na huenda idadi hiyo ikatimia waangaliza 250 walioitishwa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud