Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi ya Jalozai yakabiliwa na hatari wa mkurupuko wa magonjwa

Kambi ya Jalozai yakabiliwa na hatari wa mkurupuko wa magonjwa

Shirika la afya duniani WHO pamoja na washikadau wengine kwenye sekta ya afya, shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF zikiwemo tawala za afya za mikoa wanaongoza huduma za dharura za afya kwa wakimbizi wa ndani kwenye kambi ya Jalozai na wale wanaoishi kwenye wilaya ya Nowshera.

Kwa sasa huduma za afya zinahitaji kuimarishwa kwenye kambi zikiwemo huduma za matibabu dhidi ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kuendesha magonjwa ya ngozi , macho , ugonjwa wa bumu na mengineyo. Pia kuna mahitaji ya kuboresha huduma za afya ya uzazi, upangaji uzazi , huduma kwa watoto wanaozaliwa pamoja na tiba kwa magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya ngono. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)