Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na UNODC washirikiana kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

IOM na UNODC washirikiana kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa ya kulevya na  uhalifu UNODC kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wanatarajiwa kusaini makubalino hii leo yenye lengo la kukabilina na usafirishaji haramu wa watu na wahamiaji na pia katika kuboresha usimaizi kwenye mipaka.

Makubaliano hayo yatatiwa sahihi na kati ya mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing na mkurugenzi wa UNODC Yury Fedotov pembeni mwa mkutano kuhusu usalama kwenye mipaka ya eneo la kati kati mwa Asia mjini Vienna. Makubaliano hayo yanalenga kuboresha ushirikiano na shughuli kati ya mashirika hayo mawili. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)