Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii Angelina Jolie ataeuliwa Mjumbe Maalumu wa Kamishina wa Shirika la UNHCR

Msanii Angelina Jolie ataeuliwa Mjumbe Maalumu wa Kamishina wa Shirika la UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limemteua balozi mwema wa shirika hilo Angelina Jolie kuwa mjumbe maalum wa kamishna mkuu wa shirika hilo Antonio Guterres. Kwenye wajibu wake mpya mjumbe huyo mpya ataangazia athari zinazotokana na kuhama kwa idadi kubwa ya watu ambapo pia atamuwakilisha Gutteres kwenye shughuli za kidiplomasia.

Wajibu wa Bi Jolie kama balozi mwema kwenye shirika la UNHCR kwa muda wa miaka kumi iliyopita umetajwa kuwa zaidi ya wajibu wake. Edrian Edwards kutoka UNHCR anafafanua zaidi wajibu huu mpya wa Bi Jolie.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)