Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waelezea wasi wasi uliopo kutokana na mashambulizi ya angani yanayoendeshwa Sudan Kusini

UM waelezea wasi wasi uliopo kutokana na mashambulizi ya angani yanayoendeshwa Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS unasema kuwa mashambulizi ya hivi majuzi nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya watu wanane na kuwajeruhi wengine 22.Ujumbe huo umeelezea wasi wasi uliopo kuhusiana na hatma ya raia kwenye majimbo ya Unity na Warrap. Corine Momal-Vanian ni msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva

(SAUTI YA CORINE MOMAL-VANIAN)

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasi wasi uliopo kutokana na kuendelea kuongezeka kwa wanajeshi kati ya mpaka wa nchi hizo mbili ambapo amewataka viongozi wa Sudan na Sudan Kusini kudumisha amani.