Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aonyesha wasiwasi wake kutokana na kuendelea kwa mkwamo wa kisiasa Guinea-Bissau

Ban aonyesha wasiwasi wake kutokana na kuendelea kwa mkwamo wa kisiasa Guinea-Bissau

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka  yake kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Guinea-Bissau ambako viongozi waliotwaa madaraka kwa nguvu wanazidi kupuuzilia miito toka jumuiya za kimataifa inayowataka kurejesha utengamao wa kisiasa.

Viongozi hao pamoja na kupata ubinyo toka duru za kimataifa inayowataka kuheshimu matakwa ya kikatiba, lakini wameendelea kutia ngumu na kuelezea kusudio lao la kuweka utawala wa mpito.

Akilaani hatua hiyo, Ban amesema kuwa ni jambo linalodumaza machipuo mapya ya demokrasia yaliyoanza kuchomoza kwa wananchi wa taifa hilo. Amesisitiza kuwa ni tukio linalokwaza na kuharibu heiba ya taifa hilo.

Kwa mara kadhaa askari nchini Guinea-Bissau wanalaumiwa kuhusika kwenye uangushwaji wa serikali halali na kuchochea machafuko tangu taifa hilo lilipotwaa madaraka toka kwa utawala wa Kireno mwaka 1970.