Mkuu wa UM kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kingono kujiuzulu mwezi ujao

17 Aprili 2012

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ufuatiliaji wa mambo katika maeneo yaliyokumbwa na udhalilishaji wa kingono Margot Wallström, anatazamia kuachia ngazi kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa mwezi May mwaka huu kutokana na kile kilichoelezwa mambo ya kifamilia.

Wallstrom raia kutoka Sweden ambaye kwa miaka mingi amepigania haki za wanawake,aliteuliwa kwenye nafasi hiyo na Katibu Mkuu kuanzia February mwaka 2010.

Tayari Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameafiki uamuzi wa kujiuzulu kwa afisa huyo lakini katika hali ya kusikitika.

Hata hivyo ameelezea shukrani zake ambaye amemwelezea ni mtu aliyewajibika na kuleta uwajibikaji wa hali ya juu katika kipindi chote akiwa ofisini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud