Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani jaribio la Korea Kaskazini kurusha angani satellite

Baraza la Usalama lalaani jaribio la Korea Kaskazini kurusha angani satellite

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali hatua ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kurusha angani satellite yake ambayo hata hivyo haikufanikiwa.

Baraza hilo limelishutumu taifa hilo na kusema kuwa kitendo chake hicho kinavunja maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Pia limeitaka Korea Kaskazini kujiweka kando na matukio ya aina hiyo ili kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa inayopiga marafuku usafirishaji angani wa satellite za kijeshi.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice ambaye nchi yake ni rais wa mzunguko kwenye baraza hilo ametaja hatua nyingine kadhaa dhidi ya taifa hilo. Baraza hilo limetangaza kusudio lake la kuongeza vikwazo kwa Pyongyang.