Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia kutangaza Rais wake mpya

Benki ya Dunia kutangaza Rais wake mpya

Bank ya dunia inatarajiwa wakati wowote kutangaza Rais wake mpya, ambapo uteuzi utakuuwa ni baina ya watu wawili, waziri wa fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala na pendekezo la Marekani Jim Yong Kim.

Kura ya mwaka huu ni ya kwanza kwa Bank ya dunia kuchagua baina ya wagombea wawili tangu ilipoundwa zaidi ya miaka 60 iliyopita. Hata hivyo Marekani bado ina nafasi kubwa ya kuwa kiongozi mpya wa Bank hiyo.

Nchi za Muungano wa Ulaya zinaelekea kuunga mkono pendekezo la Marekani hali ambayo imeshawahi kujitokeza siku za nyuma. Ulaya na Japan kwa pamoja wana asilimia 54 ya kura zote za uteuzi wa Rais. Rais mpya atakayeteuliwa atakuwa na wajibu wa kusimamia wafanyakzi 9000, wachumi na wataalamu wa Bank hiyo.