Denmark ilishindwa kulinda haki za walofanyiwa mashambulizi ya kibaguzi:UM

16 Aprili 2012

Uongozi wa Denmark ulishindwa kutimiza wajibu wake wa kufanya uchunguzi wa mashambulizi ya kibaguzi yaliyofanywa na vijana 35 raia wa Denmark dhidi ya familia ya Kiiraq kwenye mji wa Soro imesema kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi.

Juni 21 mwaka 2004 kundi la vijana wapatao 15 hadi 20 walishambulia nyuumba ya Mahali Dawas raia wa Iraq aliyekuwa akiishi Soro na mkewe na watoto wake wanane ambao wote ni wakimbizi.

Vijana wengi waliingilia mashambulizi hayo ambapo madirisha ya nyumba yalivunjwa, mlango wa mbele kubomolewa na watu wawili akiwemo bwana Dawas wakapigwa vibaya huku vijana hao wakitoa kauali dhidi ya familia hiyo kama “nendeni kwenu.” Monica Morara anaripoti

(RIPOTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud