Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza mahakama ya India kwa kudumisha kipengee cha elimu kwenye katiba

UM wapongeza mahakama ya India kwa kudumisha kipengee cha elimu kwenye katiba

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya elimu Kishore Singh amepongeza hatua ya mahakamu moja nchini India ya kukidumisha kipengee kwenye katiba kinachohusu masomo ya bure kwa watoto.

Kipengee hiki kinaeleza kuwa asilimia 25 ya nafasi kwenye shule za kibinafsi na za umma nchini humo zitatengwa kwa watoto wasiojiweza kiuchumi. Uamuzi huo wa mahakama uliotolewa hiyo jana unajiri baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na washikadau wa kibinafsi wanaodai kuwa sheria hiyo inaenda kinyume na uhuru wao .