Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Coomaraswamy alaani kuingizwa kwa watoto jeshini nchini Mali

Coomaraswamy alaani kuingizwa kwa watoto jeshini nchini Mali

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuhusu watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy ameelezea hisia zake kuhusiana na ripoti ya kutumika kwa watoto na waasi wa Tuareg na makundi mengine ya kiislamu kaskazini mwa Mali. Coomaraswamy amesema kuwa kutumika kwa watoto jeshini ni jambo ambalo kamwe halitakubalika na kutaka pande husika kuheshimu sheria ya kimataifa.

Pia kuna ripoti zinasema kuwa wanawake na wasichana wanatekwa nyara na kubakwa huku hospitali zikiporwa. Huku hali ikiendelea kuwa mbaya, zaidi ya watu 200,000 wakiwemo watoto wamelikimbia eneo la kaskazini mwa Mali.