Vikosi vya jeshi vimeripotiwa kuchukua udhibiti nchini Guinea Bissau

Vikosi vya jeshi vimeripotiwa kuchukua udhibiti nchini Guinea Bissau

Ripoti zinasema kuwa huenda wanajeshi wamechukua udhibiti wa taifa la Guinea Bissau. Inaripotiwa kuwa hatua hizo za jeshi kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi zinajiri majuma mawili kabla ya awamu ya pili ya uchaguzi wa urais ambao waziri mkuu Carlos Gomes Jr anaonekana kuwa mgombea mkuu.

Kulingana na msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Guinea – Bissau Vladimir Monteiro ni kwamba usiku wa Alhamisi kulisikika milio ya risasi na mapigano hata kama hali hiyo iliripotiwa kuwa tofauti leo Ijumaa.

(SAUTI YA VLADMIR MONTEIRO)

Bwana Monteiro pia amesema kuwa kulishuhudiwa ukosefu wa nguvu za umeme usiku kucha.