Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha raia wanaokwenda uhamishoni toka Benin kinaongezeka:IOM

Kiwango cha raia wanaokwenda uhamishoni toka Benin kinaongezeka:IOM

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM inaonyesha kuwa kiwango cha raia wa Benini wanahamia katika nchi nyingine za Afrika magharibi kimeongezeka.

Ripoti hiyo imetaja mambo kama kukosekana kwa ajira, kuwepo wa kiwango cha umaskini, kuongezeka kwa gharama za maisha ni baadhi ya mambo yanayowasukuma raia hao kukimbilia nchi nyingine.

Takwimu kutoka idara ya Benin inayohusika na raia wanaokwenda nje ya nchi zinaonyesha kuwa kiasi cha watu milioni 4.4 wamekimbilia katika nchi za jirani.

Kulingana na mchanganuoa wa ripoti hiyo, pamoja na raia hao kwenda nchi za jirani lakini pia hukimbilia katika nchi za Ulaya.