IOM kutoa misaada kwa wakimbizi wanaokimbia mapigano kwenye jimbo la Blue Nile

IOM kutoa misaada kwa wakimbizi wanaokimbia mapigano kwenye jimbo la Blue Nile

Makundi kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini yanafanya ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na mashirika mengine ya kibinadamu katika kuhudumia idadi kubwa ya wakimbizi na ambayo inazidi kuongezeka wakimbizi wanaokimbia mapigano na mashambulizi ya angani kwenye jimbo la Blue Nile nchini Suda Kusini.

Kulingana na UNHCR zaidi ya watu 92,700 wamelikimbia jimbo la Blue Nile tangu kuanza kwa mapigano hayo mwezi Septemba mwaka uliopita huku wengi wakipiga kambi kwenye kambi za Doro na Jamman. Kwa muda wa juma moja lililopita zaidi ya wakimbizi 2800 wameandikihswa kwenye kambi ya Doro. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)