Zaidi ya watu 180,000 wahama makwao kufuatia oparesheni nchini Pakistan

13 Aprili 2012

Ripoti kutoka kwa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zinasema kuwa idadi ya watu waliohama makwao kufuatia kile kinachotajwa kuwa oparesheni ya usalama inayoendeshwa na serikali ya Pakistan kaskazini magharibi mwa nchi kwa sasa imezidi watu 181,000. UNHCR inasema kuwa watu zaidi wanaendelea kuwasili kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Jolozai karibu na mji wa Peshawa.

Kwa sasa UNHCR imesambaza misaada ikiwemo matandiko ya kulalia na vyombo vingine huku mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yakiwemo UNICEF, WHO na WFP yakitoa huduma kama vile huduma za maji na usafi, elimu ya msingi , usambazaji wa chakula na huduma za utoaji wa chanjo wakati karibu mahema mapya 4000 yameweka katika kambi ya Jolozai. Edrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud