Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani jaribio la roketi la Korea Kaskazini

UM walaani jaribio la roketi la Korea Kaskazini

Umoja wa Matiafa umelaani jaribio lililoshindwa la Korea Kaskazini la kutuma chombo angani jaribio lililofanyika mapema hii leo na kushindwa baada ya roketi iliyokuwa imebeba chombo hicho kusambaratika na kuanguka baharini dakika chache baada ya kufyatuliwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa mjini Geneva katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa jaribio hilo lilikuwa ni kwenda kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa ambalo linaipiga marufuku Korea kaskazini kutokana na kuendesha majaribio ya maroketi. Corrine Momal-Vanian ni msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

(SAUTI YA MOMAL-VANIAN)