Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia lazima ihakikishe mauaji ya kimbari hayatokei tena:UM

Dunia lazima ihakikishe mauaji ya kimbari hayatokei tena:UM

Mwaka 1994 dunia ilighubikwa na majonzi baada ya siku 100 za machafuko nchini Rwanda zilizosababisha mauaji ya kimbari. Watu zaidi ya 800,000 waliuawa wengi wakiwa Watutsi na Wahutu wa msimamo wa wastani.

Wiki hii Umoja wa Mataifa na dunia imewakumbuka waliopoteza maisha na manusura wa mauaji hayo. Kauli mbiu ya mwaka huu “kujifunza kutokana na historia ili kujenga mustakhabali bora” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema tangu zahma hiyo miaka 18 iliyopita serikali ya Rwanda imefanya juhudi kubwa katika kujenga jamii ya amani na haki, na kwamba Jumuiya ya kimataifa itahakikisha janga kama hilo halitotokea tena.

Hata hivyo amesema pamoja na hatua zinazopigwa na serikali ya Rwanda mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR imekuwa daraja muhimu la kuhakikisha haki inatendeka. Sikiliza makala hii imeandaliwa na Flora Nducha.

(FEATURE GENOCIDE)