Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari ya majanga inaongezeka duniani:Rais wa GA

Hatari ya majanga inaongezeka duniani:Rais wa GA

Watu wengi zaidi na mali nyingi hivi sasa ziko katika maeneo ambayo yana hatari kubwa ya majanga amesema Rais wa baraza kuu la moja wa Mataifa.

Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameendesha mjadala usio rasmi kuhusu upunguzaji wa hatari ya majanga kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo Alhamisi. Moja ya vitu vya kwanza alivyozungumzia ni tetemeko lililoikumba Indonesia siku ya Jumatano.

Amesema zaidi ya nusu ya miji mikubwa duniani ipo katika maeneo ambayo yana hatari kubwa ya matetemeko ya ardhi. Pia amesema kwamba tangu miaka ya 1970 idadi ya watu wanaoishi katika maeneo yanayokabiliwa na mafuriko na vimbunga imeongezeka zaidi ya asilimia 100.

Amesema ktokana na ongezeko hilo hatari ya kuporomoka kiuuchumi pia ni kubwa na hatari ya kupoteza utajiri na mali kutokana na majanga ya hali ya hewa sasa inazidi kiwango ambacho utajiri ulivyotafutwa.

Mwaka jana pekee Bwana Nasser anasema kulikuwa na maelfu ya maisha ya watu yaliyopotea , na hasara ya mamilioni ya dola za uwekezaji ktokana na majanga ya asili.