Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano na mivutano ya kijamii imepungua Darfur:UNAMID

Mapigano na mivutano ya kijamii imepungua Darfur:UNAMID

Kumekuwepo na hali ya kupungua kwa mapigano na migogoro ya kikabila kwenye jimbo la Darfur Sudan amesema mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika jimboni humo UNAMID bwana Ibrahim Gambari akizunguumza na waandishi wa habari Alhamisi mjini Khartoum.

Ameongeza kuwa pia shughuli za kihalifu dhidi ya raia zimepungua ikiwemo unyang’anyi , utekaji nyara na mashambulizi dhidi ya misafara ya misaada ya kibinadamu. Gambari amesema baada ya kusafiri katika jimbo hilo na kusikia kilio cha watu UNAMID iliongeza askari wa diria kutoka 100 hadi 160 kwa siku mwaka 2012. Na kuhusu hali ya kibinadamu amesema imeimarika na kwamba wameshuhudia idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wakirejea kwa hiyari katika vijiji vyao Magharibi mwa Darfur.